Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Vipaumbele vya huduma ya MGMT

Pamoja na yote tuyafanyayo, bado msingi wa huduma yetu ni kuihubiri injili ili watu waokoke waende mbinguni , lakini tuwafanye wawe wanafunzi wa Yesu uli waweze kwenda kuwaleta wengine kwa Yesu. Mt 28:19. Mwalimu mmoja katika chuo cha theologia nilichosoma,alisema: Kumhubiria mtu injili akaokoka ni jambo jema tena ndilo linalotakiwa na Mungu, lakini jambo jema zaidi ni kumfanya muumini huyo aweze kuwaleta wengine kwa Yesu(to multply) ili kanisa lipate kuongezeka.Mdo 2:46-47. Lakini kama tunavyoona sasa, makanisa mengi “yamewahodhi”  waumini wao na kuwafanya kama “mitaji” ya kujipatia fedha bila kuwafundisha ili wafikie kiwango cha kuwa wanafunzi wa Yesu na waweze kuwaleta wengine kwake. Wamekuwa wakihubiriwa injili ya “kistaarabu” huku wakibembelezwa na kuombwa “msamaha” kila mara hata pale inapotokea “wamechelewa” kutoka kwenye ibaada! Wanapokuwa kwenye “mambo yao”  kama kuangalia mpira kwenye luninga   na tamthilia,hakuna  anayewaomba “misamaha” kwa kuchelewa! Huu ni udhaifu mkubwa kwa kanisa kwa jinsi wanavyowaogopa watu kwa sababu ya “fedha zao” na hasa walio matajiri. MGMT, bila kujali nani yuko hapo na ana hela kiasi gani za kutoa hiyo “sadaka” tunaikemea dhambi waziwazi kwa kuwa hatuko chini ya mamlaka yeyote ya utawala zaidi ya Kristo mwenyewe. Kwa njia hii tumejenga maadui wengi upende wetu wanaotupiga vita, lakini pia tumekuwa na marafiki wa kweli wanaohubiri injili pamoja nasi kila tuendako kwa njia ya utoaji wa changizo (sadaka).

Hata huduma zingine zilizokuwa maarufu kwa injili miaka iliyopita,sasa hivi zimegeukia injili ya utoaji wa sadaka kwa kuzunguka na bahasha mijini huku wakitoa ahadi ya “toa ubarikiwe” au  “kupanda mbegu” kwa njia ya utoaji wa fedha,kama ilivyokuwa kwenye kampuni ya DECI iliyowaliza watu kwa udanganyifu wa “kupanda na kuvuna”.

Ahadi ya  kuwa “ukitoa zaidi utabarikiwa zaidi”  inamfanya   Mungu wetu kama “mfanya biashara anayeuza baraka”! Watumishi wengi wa wa siku hizi napokuwa “wamekusanya ” fedha za watu kwa njia ya bahasha,huenda kwenye miji mingine(sio vijijini) yenye watu wenye uzwezo wa kifedha kwa ratiba yao wenyewe walioipangia isiyoendana kabisa na ratiba ya Mungu. Kwa mfano, haiwezekani kila mwaka mtu akafanya mkutano na semia katika miji ileile, kipindi kilekile,eneo lilelike,kuwahubiria watu walewale, n.k ukasema huyo ni Mungu “amekutuma”. Hapa,  inatia shaka.

Kwenye huduma yetu, hatuna ratiba kamili kwa kuwa kila mara tunapokea simu toka maeneo mbalimbali mijini na vijijini wakihitaji huduma ya mikutano na semina nasi huwa tayari kuwapelekea. Kuna maeneo mengine ambayo nimeyafika, siamini kama tutarudi tena kwa sababu ya umbali na gharama zake na hasa vijijini ambako hata usafiri ni taabu kabisa. Tunapoalikwa vijijini gharama karibu zote huwa ni zetu,hatutegemei kurudi na “burungutu” la fedha,zaidi ya kupata sado ya mahindi, maharage,kuku, na “zawadi” nyinginezo.

Hebu Mungu amwezesha kila mmoja kuwa mwanafunzi wa Yesu atakayeweza kuzaa kwa njia ya kuwapandia watu mbegu ya neno la Mungu mioyoni kwao,ili izae 30,60, hata 100 badala ya kuwapandia watu “mbegu” ya kutoa fedha ili ziongezeke ambazo ni uharibifu kwani hayo ni mambo ya mwilini. Ukipanda katika mwili, utavuna uharibifu.Tunakukaribisha uendelee kuwasiliana nasi uli tuifanye kazi hii kwa pamoja kwa kuwa kila mtu atatoa hesabu yake siku ya mwisho bila kujali kuwa alikuwa mchungaji, mwinjilisti,askofu, mzee wa kanisa n.k. Nakukaribisha tena kwenye huduma ya MGMT.

Mwj. Moses E. Malugu,

Mwanzilishi na Mkurugenzi,MGMT.

 

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi