Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Shuhuda

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mungu amefanya muujiza wa ajabu katika huduma yetu. Kupitia kwa watoto wangu wapendwa wakiongozwa na Elisha, wameweza kutupatia usafiri wa  gari aina ya SUZUKI/VITARA (4 wheel drive) reg no:T 468-BTV, tarehe 26/12/2013 ambayo itatusaidia sana kuweza kuyafikia maeneo mengi kule vijijini.Thamani  ya gari hilo ni shs milini 10. Jambo ambalo tunaweze kushirikiana kulifanya ni kuhakikisha tunatoa changizo letu kila mara kwa ajili ya kulifanyia matengenezo na mafuta kwa kuwa vijijini hakuna “bahasha” ambazo tunaweza kuja nazo ili kukidhi gharama za kuendesha gari pamoja na huduma zingine. Kila mara tutakapokuwa tunasafiri ni lazima kuwa na “prest” ambayo kwa vyovyote vile ni lazima kuwe na fedha ya kuniwezesha kusafiria.

Mungu ni mwema, tunatazamia atufanyie mambo makubwa zaidi kuliko haya ambayo ameendelea kutufanyia, tumeomba usafuri muda mrefu tukaona kama hatupati, lakini muda ulipofika, Bwana alitupa. Usikate tamaa katika kuomba kwako, lakini mara nyingi subiri wakati wa Bwana ufike kuliko kung’anga’na mpaka “kieleweke” kama tunavyofundishwa na baadhi ya waalimu wa maombi.

Mwaka huu wiki ya mwisho ya mwezi wa kwanza tunatarajia kwenda Pemba na Zanzibar kwa huduma, watumishi  wa huko wanahitaji sana Biblia na vitabu mbalimbali vikiwepo vitabu vya nyimbo za tenzi za rohoni. Tafadhali kama unaweza kunipatia, wasiliana nami kwa njia ya e-mail au nipigie kwa no za simu zilizopo kwenye website yetu.

Kila la heri kwa mwaka wa 2014,

Ubarikiwe. Mwj Moses Malugu

2/1/2014.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Ziko shuhuda nyingi ambazo Mungu ametuonyesha kwenye kazi yake,lakini zote hizi ni kwa ajili ya kuujenga ufalme wake hapa ulimwenguni na kuwaimarisha watu katika imani ya Yesu Kristo. Ushuhuda mzuri  katika maisha ya mkristo humshinda kabisa shetani.

Kwa hiyo, ukiwa na ushuhuda wowote juu ya jambo au mambo makuu ambayo Mungu amekutendea shirikisha wengine ili nao  wainuliwe.Biblia inasema “Aliye na mwana anaushuhuda” 1Yoh 5:10-11.

Lakini nikushirikishe shuhuda chache hapa.

Mwaka 2013,mwezi wa nane tulikuwa  Kondoa kwa ajili ya kazi ya injili. Wakati wa usiku tukionyesha sinema, wenyeji walianza kutupopoa kwa mawe na kisha kutumia nguvu za giza. Kwa bahati mbaya sana mawe yale yaliwapata “watu wao” na kuwajeruhi vibaya, matokeo yake ilibidi waweke ulinzi wenyewe ili kutulinda kwani  walifanya hivyo mara nyingi lakini hawakutupata. Kila tulipopeleka malalamiko yetu kwa mhusika(m/kiti wa kijiji) hakuchuhua hatua yeyote pamoja na kwamba tulikuwa na kibali cha serikali.

Moja ya siku waliandika ujumbe wakitaka tusiendelee kuhubiri injili “kali” inayowaumiza. Wakasema “tunampa mhubiri onyo la kwanza asipopunguza ukali wake tutachukua hatua”. Kwa kuwa mhubiri nilikawa mimi mwenyewe, niliongeza “makali” mara mbili zaidi  sikuweza kuona lolote kwa kuwa nilijua kuwa vile vilikuwa ni vitisho vya shetani baada ya kumgusa katika maeneo yake. Sifa kwa Bwana Yesu.

Siku moja baadaa ya kuhubiri injili, kuna mtu alikuja na kuniambia:”Mchungaji”unajua ni kwa nini kanisa limependa fedha sana siku hizi  kuliko kuhubiri injili? Nikamwambia ni unabii unatimia maana hizi ni siku za mwisho. Akasema pamoja na hayo, ngoja nikupe siri: Umesikia jinsi ambavyo matangazo ya  kila jumapili yanayohusu watu kutoa “shukrani  ya pekee”kanisani kwa kudai kwamba kuna mambo mengi Mungu aliyowatendea?. Ukisikiliza kwa makini huwa hawasemi “wametendewa nini” na huyo Mungu, badala yake kanisa huwapokea na kuwaruhusu kutoa hiyo “shukrani ya pekee” kanisani.

Akaendelea kusema:

Kuna mtandao uliopo siku hizi na mimi nilikuwa mmoja wa mtandao ambao sasa nimeuacha baada ya kuokoka.Ktika mtandao ule,watu hujifanya kutoa sadaka ya shukrani  ya “pekee” na kuomba watu wengine wawasindikize. Kwenye “sadaka ile” maneno yahusuyo kanisa kupenda fedha hunenwa, ili kanisa lioende fedha, libaki likihubiri sadaka tu, huku liacha kabisa kuhubiri injili kama unavyoona sasa. Maombi ya kuombea ile sadaka,ili “ifanye” kazi iliyokusudiwa, huwa hayana nguvu maana mengi ni ya “kikariri” na yaliyojaa tamaa ya kupenda fedha hayavunji nguvu ya maneno yetu, ndio maana sasa kila kanisa linapenda fedha sana,  halina tena injili ya toba iokoayo.  Mtandao wetu ni mpana uko kwenye makanisa yote duniani. Kwa kuwa wachungaji wetu wengi wao wanapenda fedha kama ilivyokuwa kwa mafarisayo, hawawezi kujua au kutambua jambo hili maana ni la rohoni hutambulikana kwa jinsi ya rohoni tu mtu mwa mwilini hawezi kutambua 1Kor 2:10-16.

“Nimekupa siri hii uwaeleze na watumishi wengine”,alimalizia sentesi yake. Ushuhuda huu ni muhimu kama nawewe umeusoma kupitia tuvoti yetu, kawaeleze na wengine.

 

Tumekuwa na semina nzuri ya neno la Mungu ya watu wote iliyofanyika West Kilimanjaro – Wilayani Hai kuanzia tarehe 17-20/11/2013. Watu wengi waliohudhuria hawakutamani semina iishe,zaidi sana wameandaa mkutano wa injili utakaofanyika mwakani mwezi wa pili Mungu akipenda. Jambo ambalo nimezidi kujifunza ni jinsi watu walivyo na kiu ya mafundisho sahihi ya neno la Mungu kuliko wakati mwingine.Mafundisho mengi ya siku hizi yamekuwa ya upande mmoja tu, utoaji kila siku mpaka watu wamechoka, wako hoi. Mtu hawezi kutatuliwa matazizo  yake na Mungu kwa kumtolea sadaka ya mafungu ya kumi. Maan ayke ni kwamba, Mungu hana shida na sadaka ya mafungu ya kumi ilipo kuwa “watu’ ndio wenye shida hiyo. Heby tuwahubirie watu neno la Mungu na kuwafundisha mafundisho yaliyosahihi waweze kumjua Yesu wao wenyewe, uwezo wake, nguvu yake, upendo wake, rehema yake, mamlaka yake na sifa nyinginezo. Mtu akimjuea Mungu wa kiwango hili, hawezi kutangatanga na kutafuta msaada mahali pengine. Miuziza nayo sasa inatesa watu, watu wanafurahi wakiona “misukule” inafufuliwa sijui wanafurahia nini wakati walitakiwa kujifunza habari za Yesu Kristo.

Ni vema siku zote kujifunza habari za Yesu kuliko kujifunza habari za shetani na shuhuda zake maana hazitakusaidia chochote, zaidi sana utapata hofu pengine  utashindwa hata kulala usingizi maana huna amani.

 

USHUHUDA KWA AJILI YA SAFARI YA MBULU NA SINGIDA KUANZIA  TAREHE 5-17/11/2013.

Niliondoka terehe 5/11 kueleka Chuo cha Biblia cha Mbulu (Waama Bible School) kwa huduma ya siku tano mpaka 10/11/2013.

Somo ambalo nililifundisha lilihusu “Uinjilisti na Umisheni” kwa Mataifa tukisimamia neno la Mungu toka Mt 28:19-20. Lilikuwa somo zuri sana lililowagusa wainjilisti na waalimu wengi kwa sababu wengi wao  walifahamu nini maana ya kuwa mwinjilisti na baadae kufanya kazi ya umisheni. Uinjiliti siyo kazi ya kukaa ofisini na kungoja watu waje kama “ofisa”fulani wa kampuni, bali ni kwenda kwa watu waliopotea na kuwapelekea habari  njema za wokovu wa Yesu Kristo. Baada kufundisha somo hilo wanafunzi wengi walichangia kutoa mawazo yao. Wengi walisema kwamba kuna umuhimu wa somo hili kufundishwa kwenye vyuo vyote vya theologia au Biblia kutokana na umuhimu wake. Mooja alisema: “Kama vyuo vyote vya Biblia wangalijifunza somo hili kama tulivyojifunza sisi, Tanzania nzima ingebadilika” alisema.

Tuliona kuwa kuna umuhimu wa  kuwashirikisha na watumishi wengine toka kwenye makanisa mbalimbali ili aweze kujua nini maana ya umisheni na nani mmisionari. Lilikuwa somo la baraka sana. Baada ya hapo niliekekea Singida ambako nilifundisha somo la “Uinjilistina Umisheni kwa Waislamu”. Ni somo ambalo liliwashangaza wanasemina wengi kwa sababu hawajawahi kusikia somo hili likifundishwa mahali popote jinsi ya  kuwafikia Waislamu na kuwapa habari njema za  Yesu Kristo. Kila siku watu wamezoea kufundishwa mambo yaleyale tu  hasa  matoleo yasiyoisha. Wanasemina walibeba mzigo mkubwa na kujua umuhimu wa kujifunza somo hili ili wawapelekee waislamu habari njema. Ilikuwa semina ya pekee kwa kweli.

Jambo ambalo nimekuwa nikijifunza kila siku kwa upya ni jinsi watu wanavyopenda mafundishi ya kweli yanayogusa mioyo yao na si yale ya kuhitaji  kupokea kwa waumini wakati wote  huku  watu  wakiwa wameyachoka kuyasikia.Watumishi wenzangu, hebu tubadilike, tuwe tunamuuliza Mungu ili atupe mafundisho ambayo watu wake watajifunza mambo ya msingi  isiwe  tunalazimisha kufundisha masomo ambayo ni “interest” zao. Ubarikiwe.

 

5 Responses to Shuhuda

  • Mwaka 2002, mama mmoja aliokoka kwenye mkutano na kutoa ushuhuda jinsi alivyokuwa mchawi kwa miaka 43.Akiwa katika uwanja wa mkutano akizindika dawa zake ili watu wasiokoke wala kupokea uponyaji,alishikwana nguvu za Mungu mpaka asubuhi alipokuwa akiwa uchi.Alisema kuwa alikuwa na wenzake ambao walitoroka baada ya kuzidiwa na nguvu za Mungu.Baada ya kupokea sala ya toba alikubali kuokoka na kuleta zana “zake za kazi” vikateketezwakwa moto, akabatizwa na kuwa mkristo.

  • Mwaka 2004, Mungu alimponya binti aliyekuwa hapati choo kubwa kwa muda wa miaka mitatu, lakini alikuwa akila na kunywa bila kujisaidia na hakufa.tulipomfanyia maombi, mapepop yalitimka ndani yake yakidai kuwa ndiyo yalyokuwa yakila uchafu tumboni.

  • Mwaka 2005, mama mmoja aliyekuwa ameolewa na jini na kuzaa nalo mtoto kilema,alifunguliwa na kuachwa huru kwa jina la Yesu,baadaye motto alitoweka katika mzaingira ya kutatanisha baada ya huyo mama kufunguliwa.

  • Mwaka 2007,watu waliokoka bila kuhubiriwa injili.Wakati mhubiri wa injili anajiandaa kuhubiri, mama mmoja alienda mbele na kumwambia kuwa nanataka kuokoka.Mhubiri alimwambia arudi na kuahidi kuwa atamwita baadaye. Aliposimama, alimwita mama huyo na kutangaza kuwa kama kuna mtu yeyote atakayependa kumsindikiza mama mhuyo ili aokoke aje mbele.Wakati wombo wa kuabudu ukiimbwa, watu wengi walikuja mbele kwa machozi, wakihitaji kuokoka. Mhubiri aliwaongoza sala ya toba nawengine walipokea uponyaji wakati ule ule, na baada ya dk 15, mkutano uliahirishwa na watu wakarudi nyumbani wakiwa wameokoka na kesho yake walihudhuria semina kwa ajili ya kufundishwa neno la Mungu. Katika kijiji kile karibu watu robo tatu ya watu waliookoka kwenye mkutano ule wamesimama.Sifa kwa Bwana Yesu.

  • Thank you Ben,
    Be Blessed

Leave a Reply

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi