Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Namna ya Kushiriki/Changizo

Hatuna masharti  magumu kama mtu anataka kushiriki kwenye huduma hii ila tumeweka utaratibu fulani wa kuufuata.

Maombi: Hili ni jambo muhimu zaidi kuliko mambo yote ingawa na mengine yana sehemu yake. Hivyo, mwombe Mungu akupe kibali cha kujiunga na huduma hii, kwani kuna watu wengi wamejiunga kwa kutumia akili zao, wamefika njiani mazingira yamewashinda,wameondoka bila kuaga wengine wakinung’unika na kulalamika kuwa hawapati kitu chochote. Hivyo,muulize Mungu juu ya wito wako unaotoka moyoni mwako kabisa  ambao utausimamia katika huduma. Wito wako  utakufanya usimwangalie mwanadamu, masilahi,kunung’unika au kuilalamikia huduma baada ya kuona mapungufu ambayo hayakwepeki, badala yake utamtazama Mungu aliyekuita kupitia kwenye huduma hii  nawe utakuwa tayari  kumuuliza jambo la kufanya kila wakati utakapokuwa kwenye huduma.

Sifa muhimu sana  ya kujiunga na huduma hii ni vema  kama mtu atakuwa ameokoka  ingawa hatumlazimishi mtu kuokoka,asiwe mtu anayehubiri habari za “uzuri”  wa dini yake  na kujisifia karama kwa kuwa  huduma yetu  hufanya kazi na makanisa mbalimbali ya kumtangaza Kristo bila kuhusisha  mapokeo ya dini zao….Sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa…1Kor 1:23.

Michango ya pesa

Unaweza kuichangia huduma yetu  kwa kutuma fedha au kutoa mali yako kwa ajili ya  kazi ya Mungu. Kwa habari ya fedha, unaweza  kutoa kwa kadri  unavyopata,kwa kila wiki,  mwezi, miezi au kwa mwaka. Usifungwe na utaratibu wa kibinadamu bali Roho wa Mungu akuongoze katika kufanya hayo kwa kadri Bwana atakavyokujalia ili Kristo ainuliwe na huduma ipate kusonga mbele.

Kwa wale walioko jijini Arusha, wanaweza kufika katika ofisi zetu zilizoko katika jengo la OTTU,chumba no 132&133 block “B” floor ya kwanza  utamkuta  secretary wetu anayeitwa Mama Laizer, utamkabidhi changizo lako. Kwa wale walio nje ya Arusha wanaweza kutuma changizo lao kwa kutumia no za simu hizi:M-pesa,Tigo pesa na airtel money. +255-0784-517603, 0715-517603, 0759-357561.Kwa njia ya Bank:CRDB  Bank, tawi la Arusha kwa anwani ifuatayo: THE MINISTRY OF GOD’S MESSAGE TANZANIA,CRDB A/c no: 01J2034029100.

Kama uko nje ya nchi lakini unataka kutuchangia,basi tuma fedha kwa njia ya  Swift code wire: CORU TZ TZ, Western union, moneygram nk. (tafadhali wasiliana nasi kama umeamua kutuma kwa njia hizi).

Kujitolea

Unaweza kushiriki pia kwa njia ya kujitolea (volunteer), kwa njia ya kuja kufanya kazi ya injili pamoja nasi bila malipo kwani kila mtu anatarajia kupata malipo mbinguni kama ilivyokuwa kwa kina Petro walipomuuliza Yesu juu ya kuacha vyote na kuamua kumtumikia. Yesu akawaambia watapata mara mia hapa duniani na mbinguni pia.
Lakini pia, huduma yetu iko tayari kujenga uhusiano nawe  (Partinaship) hata kama uko nje ya nchi. Nakukaribisha
kujitoa  kufanya kazi na huduma ya yetu ya MGMT ili kufikisha malengo na makusudi yake kama  Bwana alivyokusudia.

Zawadi

Tunapikea zawadi yeyote ambayo Mungu atakugusa kutuletea. Kwa mfano, gari(hasa L/cruser kwa ajili ya safari za vijijini, pilipiki, compyuta. Unaweza kututumia  nguo, Biblia na vitabu vingine
Seti ya moja ya  vyombo vya kuhubiria na mashine ya kuendeshea sinema(projector),Printer, video camera, na zawadi nyiinginezo ambazo  tutazipeleka kwenye huduma zenye  mkubwa kama sisi hasa maeneo ya vijijini.

Kwa mawasiliano zaidi, tuandikie:mgmtza@hotmail.com au tutembelee kwenye tuvoti yetu: www.mgmtministry.org

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi