Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Makadirio ya bajeti ya MGMT

Makadirio ya bajeti kwa mwaka  2013-2014

UTANGULIZI:

Makadirio ya Bajeti  yanalenga na  kuhakikisha malengo ya kazi ya Mungu  yanafikiwa kwa ajili ya uhai wa huduma yenyewe na kuhakikisha ufalme wa Mungu unaenezwa kwa kila kiumbe. Marko; 16:16,Mt 28:19-20. Hivyo,huduma yetu  imegawanyika katika vitengo 4 vya utendaji na matumizi yake  yameelekezwa, upangaji wa bajeti kwa vitengo unawiana kulingana na uzito na vipaumbele vilivyoelekezwa kwa mwaka  wa  2013-14.

VITENGO VIKUU KATIKA HUDUMA NI PAMOJA NA:

(1) Utawala:
Kitengo hiki kinashughulikia mambo yote ya utawala, uratibu wa
mawasiliano na mipango yote ya huduma, ili kuhakikisha majukumu
yote yanatekelezwa bila kuwa na migongano au kuingiliana.

(2) Uinjilisti:
Kitengo hiki ndio hasa uti wa mgongo wa huduma kwa kuwa
imebeba jukumu zito la huduma nzima, tukizingatia kwamba ndani ya
kitengo hiki utendaji wa huduma umebebwa kwa asilimia kubwa.

(3) Huduma ya jamii:
Kitengo hiki kinashughulikia mambo ya kimwili yanayohusu jamii
ikiwa ni pamoja na elimu, afya na mahitaji mbalimbali yanayohusu maisha ya mwanadamu ya  kila siku. Yakobo; 2:15.

(4) Uinjilisti kwa Waislamu:
Kitengo hiki kinashughulika na mafunzo ya semina kwa Wachungaji,Wainjilisti, viongozi wa makanisa  mbalimbali jinsi ya kuwafikia Waislamu kwa njia ya mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu ili wapate kuokolewa…Mt 28:19. Kwa bahati mbaya sana, ni jambo la lisikitisha kabisa  kuona kwamba kanisa halihangaiki na Waislamu wakiwaona kama  wataenda wao  wenyewe mbinguni bila kuhubiriwa. Hata kwa wale wanaokuwa wamejitolea kuifanya kazi hii, kanisa haliwapi  msaada wowote, badala yake wanaonekana kama wanafanya kazi nyingine isiyo ya kanisa. Lazima kanisa lijue kwamba Kristo alikuf a kwa ajili ya watu wote wenye dhambi pamoja na Waislamu pia. Ni juu yetu kuwaendea kwa upole na upendo ili tuwape habari njema zenye matumaini ya uhakika za uzima wa milele. Huduma yetu inashughulika na kitengo hicho kwa kutoa mafunzo maalumu kwa  watumishi wanaofanya kazi ya Mungu kwenye maeneo ya Waislamu wengi. Unaweza kuwasiliana nasi ili utualike au tukupe  mwongozo wa jinsi ya kuwashuhudia tusiwaogope au kuwadharau.

Bado hatujaweza kujenga ofisi yetu wenyewe bado tumepanga tunailipia kila mwezi. Lakini mipango inaendelea ya kupata ofisi yetu wenyewe baada ya muda si mrefu.

(I) UTAWALA:
1. Kodi ya ofisi 100,000 x miezi 12 x2= shs………. milioni 2,400,000/=
2. Umeme/maji 50,000 x miezi 12 = shs………. 600,000/=
3. Karatasi/shajala = shs………. 500,000/=
4. Usafiri  wa gari la ofisi = shs………. 500,000/=
5. Mawasiliano 100,000 x miezi 12 =shs………mil 1,200,000/=
6. Gharama ya Vikao  x 4 kwa mwaka =shs………. 400,000/=
7. Dharura =shs………500,000/=
8. Ununuzi wa samani kwenye ofisi mpya:

(i) Meza 2 x 150,000 = shs……… 300,000/=
(ii) Computer 2 = shs……… 800,000×2 1,600,000/=
(iii) Viti 4 x 100,000/= = shs……….. 400,000/=
(iv) Calculator = shs……… 150,000/=
(v) Shelve = shs……… 300,00,0./=
Jumla ndogo = shs. …..8,850,000/=(Milioni nane laki nane na hamsini elf)

2. KITENGO CHA UINJILISTI
2.1 Mikutano:
2.1.1. Kukodi vyombo 200,000 x 8 siku x 8 = 1,600,000/=
2.1.2 Nauli/wahudumu 50,000 x watu 10 =500,000/=
2.1.3 Posho 50,000 x watu 10  500,000/=

2.2. Semina:
2.2.1 Kukodi vyombo 200,000 x siku 8 mil 1,600,000/=
2.2.2 Usafiri  540,000/=
2.2.3 Posho 50,000  siku 8= 400,000/=

2.3 Uinjilisti kwa njia ya mahubiri kwa Radio (dakika 30) 300,000xwiki 52 = 7,800,000/=
2.4 Kununua tracks, vitabu, Bibilia = 800,000/=
2.5 Ada ya Mafunzo kwa Wainjilisti = 500,000/=
2.6 Ufuatiliaji baada ya Uinjilisti = 2,000,000/=
Jumla ndogo =16,240,000/=( milioni 16 mia mbili arobaini)

3. Kitengo cha huduma ya jamii.
3.1 Gharama ya Elimu kwa watoto yatima:
3.1.1 Ada Form 1 – IV Watoto 5 x 200,000/= = 1,000,000/=
3.1.2 Mavazi ” 5 x 50,000/= = 250,000/=
3.1.3 Madaftari/vitabu ” 5 x 50,000/= = 250,000/=

3.2 Wajane na maskini = 1,000,000/=
3.3 Semina za Ukimwi – semina 6 x 200,000/= = 1,200,000/=
Jumla ndogo = 3,700,000/=

Kitengo cha Uinjilisti kwa Waislamu
4.1 Vitabu, tracks, Biblia = 500,000/=
4.2 Nauli – watu 2 x 100,000/= x 4 = 400,000/=
4.3 Posho  2 x 50,000/= siku 5 x 4 = 1,000,000/=
4.4 Dharura = 200,000/=
Jumla ndogo = 1,000,000/=

JUMLA KUU = 3,100,000/=

Maono ya huduma ya  MGMT:
Huduma ya  MGMT ina maono wa kuanzisha radio ya Kikristo ambayo itakuwa Mkoani Singida, lengo ikiwa ni kuwafikia watu wengi zaidi kwa njia ya mahubiri ya neno la Mungu. Makisio ya jumla ya gharama ya kuanzisha kituo yanafikia kiasi cha Tshs. 70,000,000/= (millioni sabini) au zaidi. Tafadhali tusaidie kututafutia wafadhili wa ujenzi wa mnara redio mara baada ya kututembelea katika  tuvoti  yetu na kuangalia  bajeti yake. Hapa chini  baadhi ya  vifaa vifutatavyo vya studio vinahitajika.

1. EXITER 1 , FM TRANSMITER 500 W/Z KWTS
2. AMPLIFIRE
3. STL
4. ANTENNA
5. SPICITEN
6. FEEDER CABLE
7. CONNECTIONS
8. TOWEN
9. BROADCAST PA I W 1 OR 2 KW FM AMPLIFIRE
10. STL LINK BW BROADCAST T X 25 BAND I STEA-10
11. ANTENNA RF TECHN/QUES 1.5
12. CONJOLE MIXER & OXYGEN
13. MICROPHONE B 2

VIFAA VYA STUDIO:
1. AUDIO CONDOLEA MIXEA
2. MICRO PHONES
3. COMPUTERS
4. G.D PLAYER (DECKS)
5. SOUND PROOF MATIHANALS
6. D J PLAYER
7. NYUMBA KWA AJILI YA RADIO STATION

Huduma pia inampango wa kujenga ukumbi mkubwa wa kufanyia semina za neno  la Mungu mkoani Singida na studio ya kurekodia nyimbo za kwaya mbalimbali.Tunategemea kutumia zaidi ya shs mil 500. Mchakato umeshaanza,tunahitaji maombi yako na kutuchangia pia kwa kadri Bwana atakavyokuwezesha. Tunatamani uwashirikishe na watu wengine ili tuweze kusaidiana kwa pamoja kama hekalu la mfalme Sulemani lilivyojengwa kwa michango ya “dunia nzima” kwani kila aliyesikia ujenzi ule alichangia kiasi cha yeye (mfalme) akasema sasa “inatosha” msilete tena, hakufanya harambee! Soma vitabu vya wafalme katika Biblia.

MAPATO:
Ili huduma iweze kujiendesha MGMT inategemea michango ya watu mbalimbali wafuatao ili kufanikisha majukumu yake kama yalivyoonyeshwa hapa chini.

1. Wafadhili na marafiki waliopo nchini
2. Changizo  la kwenye mikutano na semina(ingawa ni shida sana kupata huko vijijini)
3. Changizo  toka kwa wanachama wa MGMT,
4. Changizo  toka vikundi vya makanisa mbalimbali na watu binafsi
5. Uuzaji wa vitabu na maandiko.

Huduma inapenda kuwashukuru wale wote wanaoendelea kuitegemeza kwa maombi na michango yao.  Watu wengine wamekuwa hodari kuchangia sherehe za arusi,kipa imara,sendoff, kitchen party, na nyinginezo  kwa mamilioni ya fedha lakini hawataki  kuichangia kazi ya Mungu au kusomesha watoto wao.

Kwa wakati huu,huduma  imezidi kupanuka  kila siku kwani watu wengi sasa wanahitaji injili kuliko ilivyokuwa huko nyuma na kufanya nguvu kubwa kuhitajika zaidi ya fedha na mali pamoja na maombi.Tunamshukuru Mungu kwa hilo.

Tunazidi  kukuomba  uendelee kuiunga mkono huduma hii kwa maombi na utaratibu wa changizo tuliokuwekea. Kwa wewe ambaye hujaifahamu huduma  yetu na unahitaji kujiunga, nakukaribisha sana  jina la Yesu  Kristo,uwe nasi sasa. Tumekwisha kukueleza namna ya kutoa changizo lako kwenye ukurasa wa  jinsi ya kushiriki/changizo.Karibu sana na Mungu akubariki.

Ni mimi Mwinjilisti Moses E. Malugu,

Mkurugenzi na Mwanzilishi wa huduma-MGMT.

 

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi