Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Log In

Ushuhuda wa kazi  ya ufuatiliaji (follow-up)iliyofanyika  Kondoa kuanzia tarehe 26/11-4/12/2013.

Huduma ya MGMT ilituma timu ya ufuatiliaji wa kazi ya  ajili ya mkutano wa injili uliofanyika kuanzia tarehe 22-29/9/2013. Kiongozi wa timu alikuwa mama Mwinjilisti Magdalena Malugu. Timu ile ilikuwa na kina mama 5 kutoka Arusha wengine walijiunga na timu yao wakiwa wenyeji.

Anasimulia jinsi walivyokutana na mambo magumu ukiwepo ugumu wa maisha ya watu wanaotaka kumpokea Yesu maishani mwao wengi wao wakiwa waislamu. Waliweza kutembelea zaidi ya nyumba  15 wakishuhudia injili kwa watu wasiomjua Yesu, wengi walikuwa tayari kumpa maisha Bwana Yesu lakini kuna waliokuwa wanatishwa na sheria za dini yao kwamba wakiacha uislamu watalaaniwa au kufukuzwa kijijini. Walikubali tu kuombewa na kukubali  kwamba wameguswa na neno la Mungu, wanatafuta namna ya kujenga mazingira ya kwenda kanisani ili wakabatizwe hata kama ni kwa siri ili wawe wakristo.

Jambo lingine walilokutana nao ni ugumu wa maisha, na hasa ya kiuchumi  na umasikini wa kutisha. Walifika mahali wakaishiwa fedha za matumizi kwani waliweza kuwafadhili kina mama ambao walikuwa na hali ngumu ya maisha ikabidi waagize msaada mwingine tukaweza kuwatumia ili ziwasaidie angalau nauli ya kurudia.

Hii ni changamoto kubwa kwa kanisa kwani tumesahau sana kuhubiri injili kwa mataifa kama Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo alivyoagiza badala yake tunahubiriana wenyewe kwa wenyewe kila jumapili na kuridhika. Huduma inahitaji saana mchango wako wa mali na fedha kwa kuwa tunakoenda vijijini huwa hakuna bahasha huko, zaidi sana unatoa wewe sio unapokea kama ilivyozoeleka mijini. Nenda kwenye ukurasa wa  namna ya kuchangia huduma utapata maelezo nawe utakuwa  tayari kufanya kile kile ambacho Mungu atakuwa amekujalia.

Ubarikiwe.

Ni mimi

Magdalena  Malugu,kiongozi wa timu ya ufuatiliaji-Kondoa.

Mungu awabariki.

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Join 798 other subscribers

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi