Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Kuhusu Mwanzilishi

This slideshow requires JavaScript.

Mwanzilishi wa huduma na mbeba maono  ni Mwinjilisti Moses E. Malugu.Kabla ya kuanza huduma hii, alikuwa akifanya kazi ya kuajiriwa, na mara ya mwisho alikuwa akifanya kazi kwenye sekta ya utalii kwa miaka 23 akiwa Dereva kiongozi wa watalii (Driver Tour Guide) katika mbuga za wanyama.Yesu  alimwokoa mwaka wa 1989 mwezi wa 11 tarehe 7,ndipo Mungu alimpa maono ya kupeleka injili vijijini, kazi aliyoianza rasmi mwaka wa 1998 Octoba baada ya kuacha kazi ya kuajiriwa. Anaendelea na wito wa kumtumikia Mungu  mpaka leo akiandaa semina mbalimbali maeneo ya vijijini mijini akishirikiana na huduma na makanisa mbalimbali na timu ya Wainjilisti walioko  kwenye ofisi yake.

Wakati Mwinjilisti anaacha kazi ya ajira mwaka wa 1998,alikuwa akilipwa mshahara wa shs 200,000(laki mbili) kwa mwezi na pia alikuwa na uwezo wa kutengeneza marupurupu ya zaidi ya shs milioni 1 kwa mwezi kutokana na “night allowances” na “bakshishi”(tips) toka kwa wageni na mapato mengine  halali aliyokuwa akiyapata.

Tangu alipoitwa na Mungu na kupewa huduma hii, hajawahi kupata mshahara kwani “ameajiriwa” na Mungu anapata “mshahara” toka kwake.Anashughulika na biashara ndogondogo na ufugaji wa ng;ombe wa maziwa.Ameweza kusomesha watoto 3 wakafikia elimu ya  vyuo vikuu na sasa wameajiriwa na wanafanya kazi. Yeye amesoma katika chuo cha Theolojia cha uinjilisti cha Oldonyosambu kwa miaka mitatu na kutunukiwa cheti(1999-2001) na kisha akaendela kusoma katika chuo kilichoitwa AFMINI(African Ministries Network) kwa miaka minne na kutunukiwa shahada katika fani ya uongozi na utawala wa kiroho (Spiritual Leadership & Administration).Naendelea kusoma zaidi ili aweze kupata “masters” katika chuo kikuu huria cha theologia.

Mwj. Moses Malugu ameoana na Magdalena, ana watoto watano, wanne wa kiume na mmoja wa kike.Ana wajukuu watatu wote wakike.

Pamoja na kuwa Mwinjilisti na mwalimu wa neno la Mungu, pia ni mwandishi wa vitabu mbalimbali,tayari ameandika kitabu kinachoitwa “Uchaguzi wa busara katika mtazamo wa ki-biblia na fukuto lililoko katika mfumo wetu”,kitabu kilichowasaidia sana watu wengi katika uchaguzi wa mwaka 2010 kuchauga viongozi kwa njia ya kufuata maandiko matakatifu yaani Biblia, na sasa ameandika kingine kinachoitwa LOLIONDO KWA BABU alichokitoa mwaka 2013,  ni kitabu chenye changamoto nyingi kuhusu “huduma ya babu” ambayo iligeuka kuwa “janga” kwa baadhi ya watu waliokunywa kikombe. Unaweza kupata nakala za vitabu hivi kwa kuwasiliana naye kwa njia ya e-mail:mgmtza@hotmail.com Yuko mbioni kutoa vitabu vingine kwa kadri Mungu atakavyomjalia kikiwepo cha Mjue Roho Mtakatifu, Lijue taifa la Israeli,Tumeokolewa kwa neema tu,na vinginevyo. Ameweza kutoa kanda za mafundisho kwa njia ya CD na DVD ya masomo mbalimbali.

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi