Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Kuhusu huduma ya MGMT

KUHUSU HUDUMA

IMANI YETU:

– Tunaamini kwamba kuna kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya kukiri na kumwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wetu (kuokoka)Rumi 10:10
– Tunaamini juu ya Utatu Mtakatifu na utendaji wake
– Tunaamini ufufuo wa Yesu Kristo na kuwa kuna hukumu ya mwisho kwa kila mwanadamu alioko juu ya uso wanchi
– Tunaamini kuwa kuna haja ya kila mtu kuisikia injili habari njema iletayo wokovu kabla ya kurudi kwa Yesu mara ya pili Mat 24:14
– Tunaamini ubatizo wa maji na wa Roho Mtakatifu Yoh 3:1-7,Yoh 1:33.
– Tunaamini Biblia ni neno la Mungu lililo hai, na mtu akiliamini atapata uzima ndani yake.

MTAZAMO WA HUDUMA:
– Tunatamani kila mtu afikiwe na injili habari njema kwenye mikutano ya injili, masokoni,kwenye stendi za magari,nyumba kwa nyumba na kuwafanya watu wengi kuwa wanafunzi wa Yesu zaidi Yoh 4:35
– Kufanya kazi ya kuzishauri ndoa ili ziwe na amani kwani ndizo hasa zinajenga msingi wa kanisa,
– Kuhakikisha kuwa vijana wanapata mafundisho mazuri ya kuwajenga ili wawe kanisa bora la baadaye,
– Kujitahidi kuwatunza yatima, wasiojiweza,masikini,wenye njaa kama Yesu alivyoagiza Mt 25:34-40.

Timu ya Uinjilisti.

Picha unayoiona ni timu ya Wainjilisti wa MGMT ambao huenda huko na huko vijijini kwa ajili ya kuhubiri injili kama Yesu alivyoagiza. Mt 28:19-20.

Evangelism Team
Katika picha hii, Wainjilisti wa MGMT akiadhimisha miaka 10 tangu huduma ianze tarehe 31st October 2007  wakiwa pamoja.
the cattle pulling

Hapa ni safari ya uinjilisti kwenye maeneo ya vjijini ambako injili inahitajika sana. Hili ni eneo la  Singida vijijini  kijiji cha  Kitumbili  tukisafiri kwa mkokoteni wa kuvutwa na ng’ombe.

 air meeting in the rural areas

Hii ni sehemu ya mkutano wa injili uliofanyika eneo la Upareni Gonja June mwaka 2007. Inaonyesha jinsi watu walivyo na kiu ya injili maeneno ya vijijini ambako watumishi wengi hawataki kwenda kwa sababu mbalimbali ikiwepo kupenda kufanya kazi mahali penye “mapato” kwa maana ya sadaka ili akimaliza aondoke na “burungutu” la hela. Yesu alihubiri injili mijini na vijijini bila kuondoka na “burungutu” la fedha.

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi