Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Kuhusu itikio la watu(Respond).

ITIKIO LA WATU KUHUSU INJILI:

Watu wengi wameokoka kwenye mikutano ya injili, semina mbalimbali,uinjilisti wa nyumba kwa nyumba, na mtu kwa mtu.

Watu wengi wamefunguliwa kutoka katika nguvu za giza, na kuponywa magonjwa sugu yaliyowatesa kwa muda mrefu kwa jina la Yesu Kristo.
Ndoa nyingi “zimepona” kwa jina la Yesu na kuwa na ushuhuda mzuri kwa ajili ya Kristo.

Tumepata mialiko mingi  nchini hasa maeneo ya vijijini  jambo ambalo limetufanya tuwe na muda mdogo sana “wa kupumzika”.

Watu wengi wamejiunga na huduma hii kwa njia mbalimbali kwa kutuombea, hali wengine wakijitoa kwa mali na fedha zao kutuchangia.Unaweza pia kujiunga nasi kwa njia ya changizo la wiki,mwezi, kila mara kwa kadri utakavyojaliwa kupata na Mungu,na hata kututembelea au kutuandikia na kutupigia simu kwa kututia moyo kwa kazi hii ngumu tuifanyayo.

IDADI YA MIKUTANO NA SEMINA ZA NENO LA MUNGU TUNAZOWEZA KUZIFANYA KWA MWAKA
Huweza kufanya mikutano isiyopungua 19 na semina 26. Watu wengi huokolewa na kuponywa magonjwa yao na Yesu Kristo.Wengine hubatizwa na kuwa wakristo toka kwenye imani za dini za kipagani.

MAENEO TUNAYOYAHUDUMIA:
Tunuhudumia maeneo yafuatayo kwa injili na mafundisho:
Vijijini, shule za msingi, Sekondari, Vyuo na makanisa mbalimbali kutokana na mialiko tunayopewa ndani na nje ya nchi.
Masomo yaliyofuyndishwa ni pamoja na:
Ukimwi, semina ya vijana, kuijua imani ya kikristo na kumtumimia, Roho Mtakatifu, maombi,wakili katika mtazamo wa agano la kale na agano jipya,na mengineyo.

Tumekuwa tukifundisha neno la Mungu kwa njia ya sinema hasa maeneo ya vijijini ambako watu wengi hawajui hata sinema ni kutu gani. Watu wengi wameokolewa kupitia mafundisho ya sinema hasa maeneo ya Waislamu.

Kuna gharama kubwa ya ufuatiliaji kwa kuwa  baada ya kuokoka watu wanahitaji kulelewa kiroho ili wakue. Gharama hizi zinahitaji kuchangiwa ni kila mwenye mzigo wa injili ya vijijini. Waswahili walisema “kuzaa si shida,kulea ndipo penye kazi” Nami nasema, kuokoka si shida, penye kazi ni namna ya kuukulia wokovu kwa mtu alioupata maishani mwake, na hapo ndipo penye kuhitaji malezi,ndipo penye gharama.

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi