Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

Huduma ya Ngara

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Timu yetu wa MGMT ilikuwa ha huduma eneo la Ngaremtoni kwenye kanisa la K.K.K.T ambako tulialikwa kwa semina ya neno la Mungu. Timu iliyoshiriki ni pamoja na  Mwj. Steven Kajiru ambaye alikuwa mhutubu wetu, mimi nilifundhisha somo la maombi kwa wana maombi, Mwj Israeli Kisirei na Mwj. Julius Samwel aliendesha vipindi vya maombi. Tunawashukuru wote walioiombea ile semina na sisi wenyewe kwa kuwa tuliuona mkono wa Bwana ukitenda kazi pamoja nasi. Zaidi ya watu 200 walimpa Yesu maisha yao na wengi kufunguliwa katika nguvu za giza na kuwekwa huru.  Siku mbili za mwisho tuliona Mungu akiwahudumia zaidi watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano mpaka wanafunzi wa primary na sekondari.Wengi walilipuka mapepo kuliko unavyoweza kudhani  lakini Bwana Yesu akawafungua.Semina ya waliookoka inaanza kesho tarehe 4/11 kuanzia saa 10. Watu wote waliookoka pamoja na wengine wambao wameokoka siku nyingi wanakaribishwa. Kutakuwa na maombi pia

Barikiwa.

One Response to Huduma ya Ngara

Leave a Reply

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi