Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

malugu

1 2 3 7

Huduma ya Kondoa

Wapendwa katika Kristo Yesu

Napenda kuwatangazia kwamba kuanzia tarehe 7-23/9/2019 nitakuwa Kondoa pamoja na baadhi ya wanatimu kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Uinjilisti na umisheni tuliyoifanya mwezi uliopita.  Maeneo yale ni magumu  kwa sababu ya ndugu zetu wanaokaa huko hivyo maombi ni muhimu. Pia kuna kanisa limeanzishwa eneo lile lakini Mwinjilisti  aliyepewa kusimamia bado hajapata uzoefu anahitaji kupata mafunzo yatakayomsaidia  kupambana na mazingira magumu ya umisheni. Mimi nimejitolea kufanya kazi hiyo nimepanga kurudi mara 1 kila mwezi, mpaka Decemba nitakua nimerudi mara 4. Nahitaji sana maombi yenu lakini pia kama Bwana akikugusa kwa habari ya changizo, fanya kama kwa Bwana. Unaweza kutumia no za simu zifuatazo 0784-517603,0759-357-561,0751-157-603.

Barikiwa na Bwana Yesu,

Mwj Malugu.

Safari ya Nairobi

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Namshukuru Mungu kwa ajili ya kuniombea. Nilikwenda kwenye kongamano la huduma inayoitwa Victory World Outreach toka nchini Marekani. Kongamano lilikuwa zuri Mungu ni mwema lilianza tarehe 10-24/9. Hata hivyo ninajiandaa kurudi Kondoa kijijini kwa kazi ya uinjilisti na umisheni kuanzia  tarehe 7-23/ 9. Tuzidi kuombeana na mbarikiwe.

Mwj. Malugu.

TELM

Wapendwa nawasalimu tena katika jina la Yesu.

Mkutano wetu wa TELM ulifanikiwa sana huko Dodoma, tumepanga kufanya semina mwakani itakayowashirikisha watu (na hasa vijana) umuhimu wa kuandika vitabu ili tuwe na waandishi Watanzania badala ya kutegemea kusoma vitabu vya wenzetu. Lakini pia itabidi tuhamasishane ili  Watanzania wawe wasomaji wa vitabu maana wengi wao wamebaki na mitandao ya simu tu hawafikirii kulisha akili yao kwenye kusoma vitabu. Nitawajulisha tarehe baada ya  uongozi kupanga. Jumapili tutasambaa kwenye makanisa mbalimbali ili kuifahamisha TELM kwa wakristo wetu, j3 nitaondoka kuelekea Singida ambako nitakua na huduma nyingine ya wiki moja, baadaye nitaelekea Arusha. Tunashukuru kwa maombi yenu na mbarikiwe.

Mwj Malugu.

Kikao cha TELM

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Nawasalimuni nyote katika upendo wa Mungu wetu aliyehai. Baada ya kurudi toka Manyara ambako nilikua na mkutano wa injili na semina ya neno la Mungu toka tar 12-19/8, nilielekea Dodoma kwa ajili ya kikao chetu cha Tanzania Evangelical Litreature Mission ambacho kilianza rasmi leo na kitamalizika kesho tarehe 24/8. Leo tulikuwa na somo zuri mno linalohusu namna ya kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuuza vitabu na pia namna ya kuandika kitabu kwa kutumia program ambazo tulifundishwa ili zitusaidie kwenda na wakati. Tulibarikiwa sana kwa kweli. Jumapili tutasambaa kwenye makanisa mbalimbali ili kulielimisha kanisa namna ya kuhubiri injili kwa kutumia maandiko (litreature).

Nashukuru kwa maombi yenu hasa kwa ajili ya mkutano wa Manyara, ulikuwa na baraka saaana watu wengi walibarikiwa.

J3 nitaelekea Singida kwa huduma nyingine.

Tuzidi kuombeana,

Mwj M. Malugu.

Kipindi redioni.

Wapendwa, nawasalimu katika jina la Bwana Yesu. Nina habari njema kwenu kwamba Mungu amenipa neema ya ajabu ya kufundisha kupitia redio habari maalum, kipindi kinachoitwa “Ijue kweli” kinaanza saa 1:30-2:30 uck kuanzia j3-Ijumaa. Kipindi ni LIVE unaweza kutuma ujumbe wa simu au kupiga simu  ukauliza swali tukakujibu. Siku ya Ijumaa baada ya kumalizika kwa kipindi cha Ijue kweli, naunganisha na kipindi kingine kinachoitwa “Rehema na neema” kinaanza saa 2:30-3:00. Kabla ya kipindi kwisha huwa natoa no za siku ambazo msikilizaji anaweza kunipigia akiwa nje ya nchi kwa no hizi: +255-794-517603,759357561-715517603.  E-mail malugumk@gmail.com  Kwenye facebook unaweza kusachi “habari maalum Fm” alafu on line ni: habarimaalum.radio12345.com au habarimaalum.redio123.com

Barikiwa na Bwana Yesu,

Mwj Malugu.

Mafundisho ya neno la Mungu kwa njia ya Redio

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Mungu amenipa neema ya kufundisha neno la Mungu kupitia Redio Habari maalum kuanzia mwezi wa pili mwaka huu. Kipindi changu kinaitwa Neema na Rehema, kinarushwa kila siku ya Ijumaa kuanzia saa 2:30-3:00  usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Nimepata message nyingi na maswali mengi toka kwa wasikilizaji wakitaka kujifunza zaidi kuhusu neno la Mungu. Somo ninalofundisha linaitwa “Tumeokolewa kwa Neema tu”. Tafadhali nisikilize ukipata nafasi, na kama utakua nje ya nchi unaweza kuniandikia kwa kutumie e-mail yangu malugumk@gmail.com au +255- 0784-517603,0759357561,0715-517603.

Barikiwa na Yesu,

Mwj Malugu.

 

Imani

Wapendwa watu wa Mungu,

Katika kujifunza somo la imani, kuna imani 2. Ya kwanza ni ile ya kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo, ni baina ya mambo yasiyoonekana. Ebr 11:1. Ya pili ni ile ya kusikia mambako inaambatana na imani nyingi. Rum 10:17, lakini kwa kusikia imani ya Kikristo ndio kukanyaga hatua sawasawa. Imani hizi zinafanyaje kazi kwenye maisha ya mwanadamu? Tutajifunza polepole, kwa sasa anza kujiandaa na kuuweka moyo wako tayari.

Barikiwa,

Mwj Moses E. Malugu.

Naendelea vema.

Wapendwa katika Bwana,

Nawasalimu nyote  katika jina la Yesu. Wiki kadhaa zilizopita, niliwaarifu kwamba nilikuwa naumwa, oporation niliyofanyiwa mwaka jana ya tezi dume ilivimba kwa ndani, lakini Mungu ni mwema, nimepata dawa ambazo zimenisaidia sana uvimbe umezidi kupungua, na maumivu pia. Lakini zaidi aliyeniponya ni Yesu Kristo kwani kama si yeye, hata dawa ambazo natumia hazingeweza  kuniponya. Sifa ni zake kwa kweli.Endeleeni kuniombea ili nipine, niendelee na kazi ya kumtumikia Mungu. Nawashukuru sana.

Mbarikiwe

Mwj Malugu.

Huduma ya Mazangiri

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Nawasalimu katika jina la Yesu. Huduma ya Singida kwenye kijijijicha Mazangiri ilikalizika vyema, Bwana alituhudumia mwenyewe kwa somo tulilojifunza la namna ya kufanya kazi ya uinjilisti na umisheni kwa mataifa yote.  Kwa sasa tuko Arusha, tulifika usiku wa saa 5 tukiwa salama mikononi mwa Yesu.Nawashukuru sana wale waliotuombea na kutupatia changizo lao, limetusaidia kwa ajili ya kuweka mafuta kwenye gari la huduma, wamehudumu pamoja nasi.

Tuna jiandaa kwa ajili ya huduma zingine za mwezi wa 6 na wa saba. Nitawafahamisha ratiba kamili hapo baadaye.

Mbarikiwe sana.

Mwj. Malugu.

Huduma ya Singida.

Ndugu zangu katika Kristo Yesu,

Nawasalimu katika jina la Yesu. Tutakuwa na huduma ya mkutano wa injili pamoja na semina itakayofanyika kijiji cha Kinyambuli  mkoani Singida eneo la Mazangiri kuanzia tarehe 1-8/5/2016. Tutaenda kwa kutumia usafiri wa gari ya huduma, hivyo tunahitaji maombi yako lakini pia na changizo la gharama ya mkutano ikiwa ni pamoja na mafuta ya gari tutakayoitumia. Tutakuwa timu ya wainjilisti watano toka kwenye ofisi yetu ya MGMT. Kwa changizo lako wasiliana nasi kwa no zifuatazo: m-pesa 0759-357561, airtail money 0784-517603, tigo pesa0715517603, au tuma kwenye acount yetu ya huduma o1J2034029100, CRDB bank. Nakutakia huduma njema kwa kazi ya kumtumikia Mungu.

Katika upendo wa Yesu,

Mwj Moses  E. Malugu.

MGMT.

 

1 2 3 7
Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi