Mahubiri na Shuhuda
Get Adobe Flash player

“KAULI MBIU” YA YESU KRISTO KWA ULIMWENGU WOTE:

Kwa maana nasema,wakati uliokubalika nalikusikia,siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndio sasa,tazama, siku ya wokovu ndio sasa. 2Kor 6:2.Enendeni ulimwenguni mwote; mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.Mrk 16:15.

Karibu kwenye huduma ya:THE  MINISTRY OF GOD’S  MESSAGE TANZANIA.

HISTORIA YA HUDUMA:

Huduma ya The Ministry of God’s Message Tanzania, ilisajiliwa mnamo tarehe 31/10/1997 kuwa:
Huduma inayofanya kazi kwa kushirikiana na madhehebu ya Kikristo inayofanya kazi bila faida(haizalishi) inayojitegemea,inafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MAONO:

Maono ya huduma hii ni kuipeleka injili vijijini ambako haijafika au imefika kwa sehemu ndogo, ukilinganisha na jinsi ambavyo watu wa mijini wamepokea injili mara nyingi na kutumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa makanisa ya gharama kubwa pamoja na kuanzisha miradi mingi pasipo injili huhubiriwa.

Kulea watumishi wa Mungu ili kukuza vipawa na karama ambazo Mungu ameweka ndani yao kwa njia ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya kanisa,watu waliookoka kwa neno la Mungu na kuwakuza hata kufikia kipimo cha kuwaleta wengine kwa Yesu.(Uanafunzi) MGMT,inatoa elimu kwa Wainjilisti  kwa kuwapeleka katika vyuo vya Biblia kwa masomo zaidi.

UTENDAJI KAZI:

Tunatenda kazi kwa kushirikiana na madhehebu mbalimbali ya Kikristo, mikutano mingi ya injili vijijini na kupeleka semina,pamoja na kufanya uinjilisti wa nyumba kwa nyumba.Watu wengi wameokolewa na Yesu na kupokea uponyaji.

HUDUMA :

Tunawapa watu masikini na wajane nguo na vitu mbalimbali kama madaftari na sare za shule baada ya kuwapa injili Yak 2:14-16.Kuwalea wanandoa hasa vijana wanaoanza maisha ya ndoa,na wahitaji wengine.maombi kwa ajili ya mahitaji mbalimbali kwa watu.Tunagawa maandiko na vipeperushi vyenye ujumbe wa neno la Mungu na watu wengi wamepokea na wamevisoma,wakaelewa na kubadilika.Tunahubiru injili kwa njia ya Redio kwa kulipa gharama ambayo watu hujitolea kutulipia.Injili imewafikia watu wengi kwa njia ya kusikiliza redio.

Jiunge

Weka barua pepe yako kupokea Ujumbe wa Neno la Mungu

Aina za Mada
Mada kwa Mwezi