THE MINISTRY OF GOD’S MESSAGE WEBSITE

Search

Go to content

Mwanzilishi

Kuhusu Huduma

Mwanzilishi wa huduma ni Mwinjilisti Moses E. Malugu aliyezaliwa miaka 53 iliyopita.Kabla ya kuanza huduma hii, alikuwa akifanya kazi ya kuajiriwa, na mara ya mwisho alikuwa akifanya kazi kwenye sekta ya utalii kwa miaka ipatayo 25 akiwa Dereva kiongozi(Driver Tour Guide) katika mbuga za wanyama.Mungu alimwokoa mwaka wa 1989 mwezi wa 11 tarehe 7, na baada ya hapo,alimpa maono ya kupeleka injili vijijini, kazi aliyoianza rasmi mwaka wa 1998 Octoba baada ya kuacha kazi ya kuajiriwa,kazi anayoendelea kuifanya mpaka leo akishirikiana na huduma na makanisa mbalimbali na timu wa Wainjilisti wapatao 11.Wakati Mwinjilisti anaacha kazi ya ajira mwaka wa 1998,alikuwa akilipwa mshahara wa shs 200,000(laki mbili) na pia alikuwa na uwezo wa kutengeneza marupurupu ya zaidi ya shs milioni 1 kwa mwezi kutokana na “night allowances” na “bakshishi” toka kwa wageni(tips) na mapato mengine mengi “ya halali”.Tangu alipoitwa na Mungu katika huduma hii, hajawahi kupata mshahara kama zamani kwani “ameajiriwa” na Mungu anapata “mshahara” toka kwake kwa kuwa anashughulika na biashara ndogondogo na ufugaji na kupata baraka nyingi sana.Ameweza kusomesha watoto 3 wakaifikia chuo kikuu na sasa wameajiriwa na wanafanya kazi kwenye makampuni mbalimbali na wengine wanajipanga kwenda kusoma kwa elimu ya juu. Mwj. Moses Malugu ameoana na Magdalena, wana watoto watano, wanne wa kiume na mmoja wa kike.Ana wajukuu wanne.


Mwanzo | Kuhusu Huduma | Kazi za Huduma | Shuhuda | Vipaumbele | Namna ya Kushiriki | Bajeti | Site Map


Sub-Menu:


Back to content | Back to main menu