THE MINISTRY OF GODíS MESSAGE WEBSITE

Search

Go to contentKwa maana nasema,wakati uliokubalika nalikusikia,siku ya wokovu nalikusaidia; tazama,wakati uliokubalika ndio sasa,tazama, siku ya wokovu ndio sasa. 2Kor 6:2.enendeni ulimwenguni mwote; mkaihubiri injili kwa kila kiumbe.Mrk
16:15.

Karibu kwenye huduma ya The mInistry of Godís Message Tanzanzani.

HISTORIA YA HUDUMA:
Huduma ya ďThe Ministry of Godís Message Tanzania,Ē ilisajiliwa mnamo tarehe 31/10/1997 kuwa:
Huduma inayofanya kazi kwa kushirikiana na madhehebu ya Kikristo inayofanya kazi bila faida(haizalishi) inayojitegemea lakini inafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwj. Moses E.Malugu akihubiri kwenye mkutano wa Injili

MAONO:

Maono ya huduma hii ni kuipeleka injili vijijini ambako injili haijafika au imefika kwa sehemu ndogo, ukilinganisha na jinsi ambavyo watu wa mijini wamepokea injili mara nyingi na kutumia fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa makanisa ya gharama kubwa pamoja na kuanzisha miradi mingi pasipo injili huhubiriwa.

Kulea watumishi wa Mungu ili kukuza vipawa na karama ambazo Mungu ameweka ndani yao kwa njia ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya kanisa,watu waliookoka kwa neno la Mungu na kuwakuza hata kufikia kipimo cha kuwaleta wengine kwa Yesu.(Uanafunzi)elimu Wainjilisti wa huduma hii kwa kuwapeleka katika vyuo vya Biblia kwa masomo zaidi.

UTENDAJI KAZI

Tunatenda kazi kwa kushirikiana na madhehebu mbalimbali ya Kikristo, mikutano mingi ya injili vijijini na kupeleka sinena,semina,uinjilisti wa nyumba kwa nyumb.Watu wengi wameokolewa na Yesu na kupokea uponyaji.

Tunawapa watu masikini na wajane nguo na vitu mbalimbali kama madaftari na sare za shule baada ya kuwapa injili Yak 2:14-16.kuwasomesha Wainjilisti 7 kwenye vyuo vya Biblia tangu mwaka 2001-2009 kwa gharama za ofisi.ushauri nasaha kwa wajane,waathirika wa ukimwi, wanandoa na wahitaji wengine.maombi kwa ajili ya mahitaji mbalimbali kwa watu, Mungu ameweza kusikia maombi yetu na kuyajibu.maandiko na vipeperushi vyenye ujumbe wa neno la Mungu na watu wengi wamepokea na kubadilika.injili kwa njia ya Redio

Mwanzo | Kuhusu Huduma | Kazi za Huduma | Shuhuda | Vipaumbele | Namna ya Kushiriki | Bajeti | Site Map


Back to content | Back to main menu