The Ministry Of GOD’s Message

Teachings and Testimonies

Get Adobe Flash player

Vipindi vya redio vinaendelea

Mpendwa,

Nakusalimu katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Baada ya kurudi toka kwenye safari za huduma ambako nilimalizia Singida kwa muda wa mwezi mzima, kuanzia  tarehe 10/9/2018 nitaendelea na vipindi vyangu vya mafundisho kupitia Redio Habari Maalum LIVE kuanzia saa 1:30-2:30 ucku. Kipindi kinaitwa IJUE KWELI. Ukisikiliza utapata no za studio ambazo utakua tayari kuniuliza maswali kutokana na somo nitakalokua nimelifundisha. Siku ya Ijumaa ni siku ya maswali lakini  baada ya kumaliza kipindi cha Ijue kweli saa 2:30 uck, nitaendelea na kipindi kingine kinachoitwa Rehema na Neema kinachoanza saa 2:30-3:00. Mwisho wa kipindi cha pili nimetaja no zangu za simu pamoja na e-mail yangu ambayo ni malugumk@gmail.com utaniandikia kwa e mail au utanipigia simu kuniuliza maswali au utanitumia ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Kwa wale ambao wako nje ya nchi wataanza na alama ya kujumlisha yaani +255 0784-517603,0759357561-0715517603.

Mungu akubariki na karibu sana.

Mwj Malugu.

Huduma ya Kondoa.

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Nawasalimu wote katika jina la Bwana wetu Yesu Mwokozi wa ulimwengu. Nilikuwa na huduma kule Kondoa mwezi uliopita  kuanzia tarehe 10-18/9/2017. Kazi ni kubwa sana kwa sababu  ndugu zetu wengi ni Waislamu na Wapagani wanamhitaji Yesu katika maisha yao. Nilirudi salama ingawa nina udhaifu katika afya yangu tafadhali sana naomba maombi yako ili nipate uponyaji.

Natarajia kurudi huko tena mwezi wa 11 kwa ajili ya kutafuta eneo la ujenzi wa kanisa kwa sababu hakuna kanisa lolote na eneo kubwa  ni pori. Endelea kutuombea na kuombea jambo hili ili lipate kufanikiwa.

Barikiwa na Bwana  Yesu,

Mwj Malugu.

Uanafunzi wa Yesu

Mtu anaweza kukuuliza swali hili. Nani mwanafunzi wa Yesu? Kwa sababu, Yohana alikuwa na wanafunzi wake, Mafarisayo walikuwa na wanafunzi wake, na Yesu alikuwa na wanafunzi wake pia. Sasa nani mwanafunzi wa Yesu? Unanafunzi maana yake ni nini? Je nikubatizwa? Ni kuokoka? Ni kuhamia kwenye kanisa jingine na kwenda kubatizwa huko? Ni moja ya masomo ninayofundisha kwa nguvu sana katika kipindi hiki ili kanisa liweze kuzaa kwa kuwa makanisa mengi sasa hivi hayazai tena. Hayana wanafunzi wapya, zaidi ya wale wale walioko siku zite. Majibu ya maswali haya na mengine, tutayaangalia na kujifunza katika wiki ijayo.

Barikiwa na Bwana Yesu,

Mwj. Malugu.

Bible translation

Wapendwa, Bwana Yesu asifiwe. Niko Denish Volunteer kwa ajili kazi ya kuitafsiri Biblia kwa mwaliko wa kanisa la AICT kwa kushirikiana na shirika la  Wycliffe Associate toka Marekani. Tuko zaidi ya Wachungaji 30 toka mashehebu mbalimbali. Tulianza j2 tunamaliza kesho tar 19. Tuombeeni kazi ni nzito sana.

Mbarikiwe.

Mwj. Malugu.

Huduma ya Kondoa

Wapendwa katika Bwana,

Ninawasalimu wote katika jina la Yesu. Kesho tarehe 25/2 nitasafiri kwenda Kondoa kwa ajili ya vikao vya maandalizi ya mkutano wa injili utakaofanyika mwezi wa 8 mwaka huu. Nahitaji maombi yenu.

Mbarikiwe na Bwana Yesu,

Mwj. Malugu.

Nimerudi Ars.

Ndugu zangu wapendwa,

Ninawasalimu wote katika jina la  Yesu Kristo. Nimemaliza huduma kwa ushindi mkubwa kule Bunju, sasa niko Arusha. Tarehe 29 nitaelekea Kondoa kwa ajili ya kukandaa mkutano wa injili utakaofanyika mwezi wa nane mwaka huu. Nahitaji maombi  yako na ubarikiwe.

…Mwj Malugu.

Huduma ya Mbagala

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Nawasalimu nyote kwa upendo wa Mwokizi wetu Yesu. Niko Mbagala kwa “cha tembo” kwa ajili ya huduma ya semina kwenye kanisa la KLPT. Nitamaliza tar 29 kisha nitawendelea na nyingine kwenye kanisa la Methodist Church Bunju kuanzia tar 1-5 Feb, baadaye  nitaelekea Morogoro kwa semina nyingine kuanzia tar 8-12/Feb. Nahitaji sana maombi yako na kuiombea semina kwa ujumla.

Mungu akubariki.

Mwj Moses Malugu.

Semina ya Wachungaji- Ilula

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Nawasalimu katika jina la Yesu. Semina ya Wachungaji wa madhebu yote iliyofanyika Iringa  kuanzia tarehe 3-17 imemalizika. Ilikua nzuri sana tunamshuku Mungu. Alhamisi naondoka kuelekea Dar kuna huduma nyingine ninayoanza tarehe 22- 30/1 eneo la Mbagalaela, nikimaliza nitaekea Bunju kuna huduma nyingine kwa wiki moja baadaye nitaekea Morogoro kwa huduma nyigine . Nahitaji sana maombi yako kwani huu  ni wakati wa kumtumikia Mungu.

Mungu akubariki

Mwj Moses Malugu.

1 2 3 5

Subscribe

Enter your email address to receive the God's Message to your inbox

Categories

Archives