Teachings and Testimonies
Get Adobe Flash player

malugu

Semina ya Iringa

Wapendwa, nawasalimu kati jina  la Yesu Kristo. Ninapenda kuwataarifu kuwa niko Iringa toka tarehe 2-18/1/2017 kwa ajili ya semina ya Wachungaji kwenye kituo cha Ilula Orphans Programme (IOP). Semina ni nzuri sana. Tarehe 19 nitaondoka kuelekea Dar nina semina maeneo ya Mbagala kuanzia tarehe 21-28/1 baada ya hapo nitaunganisha na semina nyingine maeneo ya Bunju mpaka tar 7 Feb. Nahitaji maombi yako kwa kweli. Mungu awabariki nyote.

Mwj Moses Malugu.

Semina ya neno la Mungu

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Kuanzia tarehe 25-1/1/2017 nitakua Meru Sing’isi kwa  ajili  ya semina ya neno la Mungu. Tarehe 2/17 nitaondoka kuelekea Iringa kwa ajili ya semina ya Wachungaji itakayoanza tarehe 3-17/1 tutakuwa waalimu 5 wawili watatoka Marekani, mmoja kutoka Kongo(DRC) mmoja toka Dar na mimi. Kila mtu atakuwa na somo lake lakini mimi nitafundisha kuhusu namna ya kufanya Uinjilisti kwa Waislamu. Nahitaji sana maombi yako kwa ajili ya semina zote. Baada ya hapo nitaelelea Dar kwa ajili ya kufundisha semina nyingine Mbagala katika kanisa la KLPT namna ya kuwafikia Waislamu kwa injili. Kama una changizo tafadhali wasiliana nami kwa njia ya simu 0759-357561,0784-517603,0715517603.

Barikiwa na Bwana,

Mwj Moses E. Malugu.

Afya yangu

Wapendwa katika jina la Yesu,

Nawasalimu nyote, kwa upendo wake Mungu. Mimi mzima naendelea na uponyaji wa miujiza ambao Bwana alinifanyia nikiwa katika hosptali ya Seliani kwa upasuaji  mwezi wa 9. Nawashukuru sana wale wote walioniombea na kuniwezesha kwa fedha zao kwa sababu matibabu yalikuwa ghali sana hasa baada ya kutakiwa kurudi mara ya pili kwa ajili ya upasuaji mwingine. Mwezi wa 12 nategemea kuwa na semina ya vijana kijiji cha Sing’isi huko Meru kwa wiki nzima. Usiache kuniombea.

Mungu akubariki.

Mwj Moses Malugu.

Huduma ya Galapo.

Wapendwa,ninamshukuru Mungu kwa ajili ya ulinzi wake, nina huduma ya  kwenda Galapo kwa ajili ya kazi ya Uinjilisti mwezi wa Novemba mwishoni, nahitaji maombi yenu. Mbarikiwe.

Mwj. Malugu.

Nimepona

Wapendwa, nawashukuru sana kwa ajili ya maombi yenu, nimepona sasa na kwa kweli niko tayari kutumika. Mungu awabariki sana.

Mwj Malugu.

Nimepona

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Nawasalimu katika jina la Yesu. Ninazo habari njema kwenu kwamba Bwana ameniponya katika ugonjwa ulionipata wa tezi dume. Baada ya kuchekiwa na Dr. ameniambia kwa kadri ya uwezo wao nimepona, ila ninajua mahali uwezo wao ulipofikia ndipo Mungu huonyesha uwezo wake usio wa kibinadamu, nami naamini kwamba kama kuna ugonjwa wowote uliobaki katika mwili wangu ambao madaktari hawakuuona au hawana uwezo wa kuutibu Bwana Yesu tayari ameshaushughulikia na mimi ni mzima kabisa katika jina la Yesu.

Mwili wangu ni hekalu la Roho Mtakatifu hakuna magonjwa yanayotakiwa katika mwili huu kwani Roho Mtakatifu hawezi kukaa kwenye mwili wenye magonjwa, yakija huyaondoa mara moja kwa sababu yeye ni Matakatifu sana. Nawashukuru kwa wote walioniombea na kuniwezesha kwa changizo, Mungu awabaiki sana.

Ni mimi katika Kristo Yesu

Mwj Moses Malugu.

Nimeruhusiwa

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Napenda kuwataarifu kwamba nimeruhusiwa jana kurudi nyumbani baada ya kufanyiwa upasuaji mwingine katika hospt ya Seliani. Hali yangu ni nzuri namshukuru sana Mungu, nikiwawashukuru pia kwa wale walioniombea na pia waliotoa michango yao kwa ajili ya matibabu. Nitarudi tena siku ya Alh tar 22/8 kwa ajili ya check up. Mungu awabariki.

Mwj Moses Malugu.

Matibabu

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Namshukuru Mungu kwa ajili ya  kunipa uzima na uponyaji baada ya kufanyiwa oporation ya tezi dume mnamo tarehe 20/7 katika hospitali ya Selian Ngaramtoni. Niko nyumbani naendelea vema na matibabu natakiwa kurudi tena hospt kwa chek-up tarehe 11/8. Nawashukuru sana kwa wale walioniombea  pia kwa wale waliotoa changizo lao  kwani matibabu yaligharimu zaidi ya shs laki 8.

Mungu awabariki,

Mwj Moses E. Malugu,

Shukrani.

Ndugu zangu wapendwa,

Nawasalimu katika jina la Yesu Kristo. Napenda kuwajulsiha kuwa nilipata ugonjwa wa kuziba mkono wiki mbili zilizopita, baada ya kupimwa ikaonekana nina tezi dume ikabidi nifanyiwe upasuaji katika hospitali ya Seliani ya N’mtoni tarehe 20/7 saa 4 asubuhi. Nilipita kwenye mapambano makali kwani shetani alitaka kuitumia nafasi hiyo kuchukua uhai wangu lakini Yesu alinipigania nikatoka  salama mikononi mwake. Nilipata ruhusa ya kurudi nyumbani jumatatu ya wiki hii niko nyumbani sasa nauguza kidonda lakini narudi kesho hosptalini  kwa ajili ya clinic. Nawashukuru sana wale walioniombea na  kutoa michango yao kwa ajili ya mtibabu yaliyogharimu kiasi cha shs laki 8. Mungu awabariki sana.

Katika upendo wa Yesu,

Mwj Moses Malugu.

Convation Dom

Wapendwa katika Kristo Yesu,

Ninawasalimu katika jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Huduma ya Dodoma Convation inaewndelea vema katika kijiji cha Kibaigwa wilaya ya Kongwa. Tunahitaji maombi yenu kwa kuwa kazi ni kubwa na mapambano ni makali.

Mbarikiwe,

Mwj. Moses Malugu.

Subscribe

Enter your email address to receive the God's Message to your inbox

Categories
Archives